Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mamia ya waandamanaji walikusanyika Paris ili kuonesha upinzani wao dhidi ya vita, ubaguzi wa rangi na dhulma ya kimfumo, na kutangaza uwepo wao katika mapambano ya kimataifa yanayohusiana na masuala haya. Tukio hilo liliandaliwa na muungano wa makundi ya wananchi.
Washiriki katika maandamano hayo walibeba mabango na bendera zilizokuwa zikionesha malengo mbalimbali ya kimataifa. Tukio hilo lilianza kwa kauli mbiu ya pamoja na wito wa amani, uadilifu na kujitawala, na wazungumzaji walisisitiza pia migogoro ya kibinadamu na ukosefu wa usawa unaoendelea kuwaathiri raia wasio wapiganaji duniani kote.
Chanzo: SAFA NEWS
Maoni yako